MBUNGE wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ leo alishangiliwa kwa kishindo na kupigiwa makofi na wabunge wenzake baada ya kutinga Bungeni kwa mara ya kwanza tangu aachiwe huru kutoa gereza la Ruanda alikokuwa amefungwa miezi mitano.

Wakati wabunge hao wakishangilia, Mwenyekiti wa Bunge, aliyekuwa akiongoza kikao hicho cha 33 cha mkutano wa 11, leo Mei 21, 2018, Andrew Chenge, aliwaomba wamalize shangwe hizo ili waweze kuendelea na kipindi cha maswali na majibu.

Sugu alitiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miezi mitano jela Februari 26, 2018 kwa kutoa lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli kwenye mkutano wa hadhara Desemba 30, 2017 katika uwanja wa shule ya msingi Mwenge, jijini Mbeya.