×

Biden Ashuhudia Chereko za Kuapishwa Kwake Akiwa Ikulu

Rais Joe Biden na mkewe, Jill Biden, wakitazama chereko za siku ya kuapishwa kwake kutoka ghorofa ya Truman ya Ikulu ya Marekani. 

RAIS Joe Biden alihitimisha chereko za kuapishwa kwake kwa kutazama milipuko ya baruti kutoka katika ghorofa ya Truman ya Ikulu ya Marekani (White House) akiwa na mkewe, Jill Biden, na watu wengine wa familia yake, akiwa ameaomba Wamarekani kuungana na kuwa kitu kimoja.

 

Milipuko ya baruti eneo la Ikulu jana Jumatano, katika kilichoitwa ‘Shangwe Marekani’ (Celebrating America) iliambatana na maonyesho ya muziki.

 

Akizungumza kwenye eneo la Kumbukumbu la Lincoln, akiwa ameapishwa kuwa rais wa 46 wa Marekani, Biden alirejea tena wito wake wa Wamarekani kushikamana kwa ajili  ya manufaa ya Marekani.

 

Fireworks are seen above the White House during the ceremony’s closing

“Ni jambo la fahari kusimama hapa na kusema maneno haya kwa heshima ya Rais Lincoln na ofisi ambayo tunaishiriki kwa ajili ya watu wa Marekani,” alisema Biden na kuongeza: “Kama nilivyosema, demokrasia ni kitu cha thamani na ni kwa ajili yenu demokrais imetawala.”

    

Leave a Comment