×

SUGU: Sistahili Kupewa Msamaha – Video

Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’  amesema kuwa hakupata taarifa kama amepewa msamaha na Rais Magufuli kutokana na kuambiwa tu atoke gerezani huku yeye mwenyewe akisema haoni kosa alilotenda mpaka kuhukumiwa kifungo.

 

Mbilinyi amesema kuwa hastahili kupewa msamaha na badala yake aombwe msamaha kutokana na madai yake kwamba hakufanya kosa na endapo alifanya kosa basi angeachwa atumikie adhabu yake. Hata hivyo Sugu amesema cha msingi ni kuwa huru kwasababu anaamini hakutakiwa kuwa jela.

VIDEO: MSIKIE SUGU AKIFUNGUKA