
WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Dkt. Charles Mwijage amewaongoza waombolezaji kuaga miili ya maofisa watatu wa Kituo cha Uwekezaji cha nchini (Tanzania Investment Center -TIC) waliopata ajali juzi maeneo ya Chalinze Pwani wakati wakielekea Dodoma kwenye mkutano.
Shughuli ya kuaga miili hiyo imefanyika katika viwanja vya Karimjee vilivyopo Posta jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na biongozi mbalimbali wa Serikali na vyama wakimemo, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Valentino Mlowola, Katibu Mwenezi wa CCM Taifa, Humphrey Polepole na wengine.

Waliofariki ni Saidi Amiri Moshi (Kaimu Mkurugenzi wa Research zamani Corporate Affairs), Zacharia Kingu (Kaimu Mkurugenzi wa Corporate Affairs zamani Investment Promotion) na Martin Masalu (Meneja Research).
Waliopata majeraha ni wawili yaani Godfrey Kilolo (Meneja wa Sheria) na dereva wa gari hilo aliyejulikana kwa jina moja tu la Priscus.