×

BREAKING: Rais Hosni Mubarak Afariki Dunia

RAIS wa zamani wa Misri, Hosni Mubarak, amefariki dunia hospitalini jijini Cairo akiwa na miaka 91. Mubarak alidumu madarakani kwa miongo mitatu kabla ya kung’atuliwa na jeshi baada ya maandamano makubwa ya raia.

Alikutwa na hatia ya kula njama katika mauaji ya waandamanaji wakati wa mapinduzi na kuwekwa kizuizini. Hata hivyo, hatia hiyo iliondolewa na akaachiwa huru mwezi Machi 2017.

Kifo chake kimethibitishwa na Televisheni ya Taifa ya Misri leo Jumanne. Mapema tovuti ya Al-Watan iliripoti kuwa kiongozi huyo alifariki kwenye hospitali moja ya jeshi ambako alifanyiwa upasuaji mwishoni mwa mwezi Januari.

Mtoto wake wa kiume, Alaa, alisema  Jumamosi kuwa baba yake yupo mahututi. Mubarak alizaliwa mwaka 1928, baadaye aliingia jeshi kama kijana na kushiriki katika vita kati ya Israel na Waarabu 1973.

Alikuwa rais chini ya muongo mmoja baadaye kufuatia ,mauaji ya aliyekuwa rais Anwar Sadat, akawa pia na jukumu muhimu katika mchakato wa amani wa Israel na Palestina.

Lakini licha ya mabilioni ya fedha  ya misaada ya kijeshi ambayo Misri ilipokea wakati alipokuwa madarakani, ukosefu wa ajira, ufukara, na ufisadi uliendelea kuimarika. Vurugu zilizuka nchi nzima  Januari 2011 kwa maandamnao makubwa kama yaliyotokea Tunisia na kusababisha Mubarak kujiuzulu siku 18 baadaye.

Leave a Comment