×

Bunge Latoa Utaratibu wa Mazishi ya Marehemu Bilago

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Buyungu, Marehemu Kasuku Samson Bilago (kulia).

Kikao cha pamoja baina ya Tume ya Utumishi wa Bunge na Kamati ya Uongozi ya Bunge kimefanyika leo na kukubaliana kuwa, mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Buyungu, Marehemu Kasuku Samson Bilago utapelekwa Bungeni jijini Dodoma siku ya Jumanne Mei 28 kwa ajili ya wabunge kutoa heshima zao za mwisho.