
MOTO mkubwa umezuka maeneo Kinondoni-Mwananyamala kwa Msisiri jijini Dar es Salaam na kuunguza banda la mashine za kuchongea mbao na nyumba kadhaa zilizopo katika eneo hilo.

Chanzo cha moto huo ulitokea asubuhi bado hakijajulikana, lakini kwa mujibu wa majirani na watu waishio karibu na maeneo hayo wamedai kwamba waliamka asubuhi na kushtuka kuona moto unawaka hivyo hatua za haraka walizozichukua ni kuanza kuuzima moto huo na baadaye kuwasiliana na kikosi cha Zimamoto ambao walifika na kudhibiti moto huo.
Kiongozi wa Zimamoto aliyefika eneo hilo aliwapongeza wananchi kwa kuchukua hatua za awali za kuzima moto huo ambapo waliweza kuzuia uharibifu zaidi wa mali hadi walipofika na kusaidia kudhibiti moto huo.