
Mwili wa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Rose Mndenye ( 31) anayedaiwa kuuawa na mume wake kwa kile kinachodaiwa ni sababu za wivu wa mapenzi umeagwa leo Kisasa mkoani Dodoma.
Baada ya kuagwa umesafirishwa kwenda kuzikwa nyumbani kwao mkoani Njombe.

Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo (UDOM) anayeshughulikia Fedha, Utawala na Mipango, Adam Mwakalobo, jana alisema alipokea taarifa za kufariki kwa Mdenye usiku wa juzi saa 4.45.
Marehemu alikuwa akifundisha chuo hicho tangu 2011 kama Mhadhiri Msaidizi wa Idara ya Utawala wa Biashara.

Mdenye alikuwa mhadhiri wa kompyuta baada ya kusoma Shahada ya Kompyuta Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kati ya 2007-10 na akasoma Shahada ya Uzamili UDOM kati ya 2013-15 hadi mauti yanamfika alikuwa mhadhiri msaidizi.
“Alikuwa akifundisha wanachuo kati ya 3,000-5000 wanaochukua kozi hiyo ambayo wamepokea kifo hicho kwa mshituko mkubwa,” alisema.
Mdenye amefariki dunia na kuacha mtoto mmoja mdogo mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu.


(PICHA NA GLOBAL TV ONLINE DODOMA)