
Mwili wa Mbunge wa Jimbo la Buyungu wilayani Kakonko mkoani Kigoma, Kasuku Bilago (Chadema), umeagwa tena leo katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma.

Viongozi mbalimbali wa kisiasa, Wabunge, ndugu, jamaa na familia nzima kwa ujumla wamehudhuria katika zoezi hilo la kumuaga mwenzao.

Akizungumza kwa uchungu jinsi ambavyo alimfahamu marehemu Bilago, Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amesema Mbunge huyo alikuwa ni zawadi kubwa kwa wananchi wa Kigoma.
