×

Fainali ya NBA ni Walewale …Warriors na Cavaliers

 

HATIMAYE timu zinazotinga fainali ya NBA zimesha­fahamika baada ya juzi Warriors na Cavaliers kushin­da michezo yao ya kanda.

Hii ni mara ya nne mfululizo timu hizo zi­n a k u t a n a k w e n y e fainali ya NBA na k u o n g e z a upinzani mkali kwa mwaka huu.

 

Baada ya timu kumaliza michezo sita kwa sare ya 3-3, Golden State Warriors walifanya maajabu baada ya kuwachapa Houston Rockets kwa pointi 101- 92 na kutin­ga fainali kwa ush­inda wa 4-3.

Awa l i i l i k u w a haiamini­ki kama timu hizo zingekwenda fainali tena mwaka huu kutokana na upinzani waliokutana nao kutoka kwenye kanda zao a m b a p o wote walifi­ka kwenye mchezo wa sita wakiwa sare ya 3-3.

 

Gold­e n S t a t e w a l ­ioneka­na kama vile wangepoteza mch­ezo huo baada ya kwenda mapumziko wakiwa wamechapwa 54- 43.

 

Hata hivyo, staa wao Stephen Curry aliamka tena kama ilivyo kawaida yake na kufanikiwa ku­funga pointi 14 kati ya 27 alizofunga kwenye mch­ezo ule.


Hii ina maana sasa Golden State watakwenda tena kwenye ukumbi wa Bay Area kwa mara yao ya nne k u w a a l i k a Cleveland Cava­liers kwenye mchezo wa kwanza wa fainali am­bayo itaanza kesho.

 

Katika mara tatu am­bazo wamekutana huko nyuma, Golden State wamefanikiwa kutwaa ubingwa huo mara mbili, huku Cleveland wakitwaa mara moja.

 

Sasa ni wakati wa Cleveland ambao wame­kuwa wakionyesha ki­wango cha juu kwa miaka ya hivi karibuni kuhakikisha kuwa wanatwaa ubingwa huo kuanzia wana­poanza harakati za kuutafuta kesho.