×

Metacha, Shikhalo Watemwa Yanga

Klabu ya Soka ya Yanga SC. imethibitisha kuachana na magolikipa wake wawili Metacha Mnata na Farouk Shikhalo baada ya kupokea mapendekezo ya mwalimu mkuu wa timu hiyo Nesreddine Nabi.

 

Kwa mujibu wa Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Haji Mfikirwa mikataba ya wachezaji hao ilikuwa inaelekea ukingoni hivyo ili kuwapa nafasi wachezaji hao kupata timu nyingine, tayari imekamilisha taratibu zote za kutemana nao.

 

Kipa namba tatu Ramadhan Kabwili atabaki ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na kocha Razack Siwa kwa makipa. Kabwili alidaka mchezo mmoja ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2020/21 ambapo ilikuwa mbele ya Dodoma Jiji. Hii ni kwa mujibu wa Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Haji Mfikirwa.

 

“Niwashukuru magolikipa hao tumekaa nao kwa kipindi cha miaka miwili lakini lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho kwa kuzingatia mapendekezo ya mwalimu kwamba tunakwenda hatua nyingine na huu ni wakati mgumu ndio maana tumewafahamisha ili maisha ya soka yaendelee.”

 

@mushigabriel,

@hotpot_tz

Leave a Comment