×

TECNO KUJA NA SIMU YA KISASA ZAIDI YA TECNO SPARK

 

KWA  mara nyingine kampuni ya simu ya TECNO ipo mbioni kuachia simu mpya ambayo ni muendelezo wa toleo la Spark ambapo simu hiyo itaingia sokoni kuanzia Juni 14 mwaka huu.

Kwa mujibu wa wadau, simu hiyo imepachikwa jina la utani la TECNO SPARK 2, kwani toleo la Spark ni moja kati ya matoleo ya TECNO yenye ushawishi mkubwa hasa ukizingatia ubora wake wa kamera na maumbo ya kuvutia.

TECNO SPARK 2 inasemekana imeboreshwa zaidi kwa mfumo wa Android ikitumia mtandao wenye kasi zaidi ya ule wa 4G.  Isitoshe,  eneo kubwa la TECNO SPARK 2 lina inchi kama 6.0 HD+ au zaidi na kioo chake kikiwa na mvuto zaidi.

 

TECNO SPARK 2 itakuwa na aina mpya ya kionjo kwenye kamera ‘MIX FLASH’ ambacho hupiga picha yenye kung’aa mithili ya kioo na inasemekana ufanyaji wake kazi ni kama flashi 3 au zaidi ya tatu. Kuhusiana na MIX FLASHI hiyo, ni dhahiri itakuwa na picha nzuri zaidi kwani inasemekana  SPARK 2 ina pixel za kamera 13+8 au zaidi.