
MOTO mkubwa umeteketeza jengo la utawala la Shule ya Sekondari Kazima katika Manispaa ya Tabora na kusababisha uharibifu mkubwa wa nyaraka mbalimbali ikiwemo mitihani ya kujipima ya kidato cha nne na cha tano.
Akizungumza na wanahabari Mkuu wa Shule hiyo Mrisho Kivuruga, amesema jengo hilo limeanza kuungua na moto majira ya saa tisa usiku wa kuamkia leo Jumamosi na kuteketeza nyaraka zote muhimu za shule hiyo ikiwemo vyeti vya wanafunzi, mitihani ya kujipima uwezo iliyomalizika juzi, chumba cha zahanati, vitabu na vifaa mbalimbali vilivyokuwemo katika jengo hilo na ofisi zake zote.
Naye Ofisa Elimu Mkoa wa Tabora Suzan Nyarubamba amesema, kufuatia kuteketea mitihani hiyo uongozi wa Mkoa utasimamia ili wanafunzi hao warudie mitihani yao.