Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) leo Juni 02, 2018 wanazungumza na waandishi wa Habari katika mkao yao makuu yaliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam. Agenda kuu ya mkutano huo ni kutaka kuzungumzia Mradi wa chuo kikuu cha kiislam kwa ufadhili wa Saudi Arabia. Aidha Bakwata wanazungumzia Suala la Baraza la EID EL-FITRI mwaka huu 1439 Hijiriyya (2018), pamoja na orodha ya Taasisi za Hijja zilizokamilisha taratibu kwa utaratibu wao.