×

YANGA YAJITOA MASHINDANO YA KAGAME CUP

Uongozi wa klabu ya Yanga umeandika barua kwenda TFF kuiomba kujitoa katika mashindano ya Kagame Cup yanayotarajiwa kuanza Juni 29 mpaka Julai 13, 2018 jijini Dar es Salaam

 

Sababu za msingi za kujitoa Kagame Cup ni kufanya maandalizi kwa ajili ya michunao ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo watacheza na Gor Mahia FC ya Kenya, Julai 18, 2018 jijini Nairobi

 

Kutokana na muingiliano wa ratiba ya Kagame Cup na Michuano ya Shirikisho, Yanga imeona ni vema kuwapatia wachezaji wao mapumziko ili kuwapa fursa ya kujiandaa vizuri

 

Katika ratiba ya michuano hiyo ya Kagame, Simba na Yanga zimepangwa pamoja kwenye kundi C ambapo kuna timu zingine ambazo ni Dakadaha ya Somalia pamoja na St. George kutoka Ethiopia