Kupitia Mahojiano Maalum ndani kipindi cha Beauty and styles Isha Mashauzi ambaye ndiye alikuwa mgeni maalum alifunguka Mengi kadiri ambavyo Catherine Kahabi alimchombeza.
Kabla ya kumuhoji juu ya maisha yake halisi Isha ametoa elimu kwa jamii juu ya Mavazi yanayopaswa kuvaliwa hasa kwa Wanawake ,lakini pia amefungukia maana halisi ya tatoo zake alizochora kwenye Mwili wake.
Mbali na hivyo amefunguka kuwa bado hajaolewa na kwa sasa yupo single kutokana na Mwezi Mtukufu wa Ramadhan na kudai kuwa Mpenzi wake sio Rasmi na kwa sasa kila mtu yuko mbali mpaka Mwezi wa Ramadhan Uishe.kujua mengi na kwa undani endelea kutazama video hii.