×

TECNO Yawafanyia Kufuru Wateja Wake, Yakabidhi Gari Mpyaaa Wengine Mafriji na Pikipiki

Meneja Masoko wa TECNO Tanzania, William Mota (kushoto) akimkabidhi funguo ya gari mume wa Bi. Sofia alipokuwa akiwakabidhi gari hiyo. Bi Sofia (mwenye baibui) akishuhudia.

 

 

 

Kampuni ya simu za mkononi ya TECNO leo imewafanyia kufuru wateja wake waliojishindia kwenye promosheni ya Vimba na TECNO Camon 17 na TECNO Spark 7 Series kwa kumkabidhi mshindi gari jipyaaa… huku wengine wakiondoka na mafriji na mapikipiki na zawadi nyinginezo.

Afisa wa TECNO, Da Bella (kushoto) akimkabidhi funguo ya pikipiki Juma Kadama baada ya kujishindia kwenye promosheni hiyo.

 

 

 

Hayo yamefanyika kwenye Hafla ya kuwakabidhi washindi hao zawadi zao kwenye ofisi za TECNO zilizopo Jengo la China Plaza lililopo Barabara ya Uhuru, mkabala na Shule ya Sekondari ya Benjamini Mkapa Jijini Dar, ambapo Bi. Sofia Suleiman ameibuka na gari jipya aina ya Suzuki.

Bi. Sofia akiikagua gari yake baada ya kukabidhiwa.

 

 

 

Wengine waliokabidhiwa zawadi zao ni Marystellah Carlos na Castro Charles waliojishindia friji kila mmoja na mshindi mwingine watatu aliyejishindia zawadi hiyo hakupata nafasi ya kujitokeza wakati wenzake wakikabidhiwa zawadi hizo. Juma Kadama yeye aliibuka na pikipiki kubwa aina ya Sunling huku wengine wakiibuka na zawadi mbalimbali.

Bi. Sofia na mumewe wakiwa ndani ya gari hiyo baada ya kukabidhiwa.

 

 

 

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi hizo, Meneja Masoko wa TECNO Tanzania, William Mota amesema kampuni hiyo ina furaha kubwa kuwakabidhi zawadi hizo wateja walioshiriki promosheni iliyoanza Julai 19 mpaka Septemba 13 mwaka huu ikiwashirikisha wateja wa nchi nzima.

Washindi wakiwa na tabasamu kwenye picha ya pamoja.

 

 

 

“Leo TECNO tunafuraha kubwa kuwakabidhi zawadi hizi wateja wetu walioshiriki promosheni hii na tunawaomba waendelee kutumia simu za TECNO ambazo ubora wake ni wa hali ya juu,” alisema Meneja Mota.

Afisa Uhusiano wa TECNO, Prisca Ernest akizungumza kwenye hafla hiyo.

 

 

 

Naye Bi. Sofia aliyeibuka mshindi wa gari amesema aliipata bahati hiyo baada ya kununua simu aina ya TECNO Camon 17 na kujikuta akiibuka na zawadi hiyo.

Juma Kadama akiwa tayari kuondoka na pikipiki yake baada ya kukabidhiwa.

 

 

 

“Jamani mimi nilinunua simu ya TECNO Camon 17 nikiwa sijui kama nitashinda chochote lakini Mungu mkubwa hivi karibuni nikapigiwa simu na watu waliojitambusha kuwa wanatoka TECNO na kuniambia nimeshinda gari.

Marystellah Carlos (kushoto) akigonga na Da Bella wa TECNO baada ya kumkabidhi friji alilojishindia.

 

 

 

Haikuwa rahisi kuamini kwani nilijua ndiyo walewale matapeli lakini walivyozidi kuniweka sawa ikabidi jambo hilo nikamshirikisha mume wangu ambapo tukaanza kufuatilia maelekezo yao kiundani ndipo tukabaini kuwa ni kweli nimejishindia gari kutoka TECNO.

 

 

“Nawaomba TECNO waendelee kuwa wakweli hivihivi kwenye bahati nasibu zao kama walivyonifanyia mimi ambaye hawanijui nami sikuwa nikiwajua zaidi ya kuona bidhaa zao,” alimaliza kusema Bi. Sofia aliyeambatana na mume wake kwenye hafla hiyo.

Leave a Comment