×

UFARANSA YAIPIGA PERU, YAFUZU

TIMU ya taifa ya Ufaransa imefanikiwa kusonga Hatua ya 16 ya Kombe la Dunia ikiwa na mchezo mmoja mkononi baada ya kuifunga Peru bao 1-0, jana Alhamisi.

 

Ufaransa ikiongozwa na mastaa kadhaa akiwemo Paul Pogba, ilipata ushindi huo licha ya mchezo kuwa mgumu ambapo mfungaji alikuwa Kylian Mbappe katika dakika ya 34 akimalizia kazi nzuri ya Pogba na Olivier Giroud.

Kwa matokeo hayo, Ufaransa imefikisha pointi 6 na kuongoza Kundi C ikifuatiwa na Denmark yenye pointi 4, zote zikisaliwa na mchezo mmoja.

 

Mchezo wa Peru ulikuwa mgumu hasa kipindi cha pili ambapo vijana hao walikuwa na makali na kuwapa wakati mgumu Ufaransa.

Katika mchezo wa mapema, Denmark na Australia zilitoka sare ya bao 1-1, huku mshambuliaji wa Denmark mwenye asili ya Tanzania, Yussuf Poulsen akipata kadi ya njano kwa kuunawa mpira ndani ya boksi na hivyo kutakiwa kuukosa mchezo wa mwisho wa Hatua ya Makundi kwa kuwa ana kadi mbili za njano.