
SAKATA la picha chafu za mke wa Dogo Janja, Irene Uwoya, zilizozua mshangao mitandaoni siku kadhaa zilizopita zikionesha sehemu kubwa ya mwili wake ukiwa wazi huku mashabiki wengine kuongea na kutoa maoni yao juu ya picha hizo, muigizaji Mwijaku aliibuka alidai kuwa Dogo Janja hana sauti kwa Ireni.
Janjaro ameibuka na kujibu tuhuma hizo huku akimtetea mkewe na kusema hata Kim Kardashian ni mke wa mtu lakini huwa anapiga picha za utupu na kuziachia mitandaoni, hivyo maisha ya staa ni tofauti na mtu mwingine wa kawaida.