
TUNISIA leo imepokea kipigo kingine katika michuano ya Kombe la Dunia baada ya kukumbana na kipigo cha ‘mbwa mwizi’ cha mabao 5-2 kutoka kwa Ubelgiji.
Katika mchezo huo wa Kundi G uliopigwa Uwanja wa Spartak, Ubelgiji wamejipatia mabao kupitia kwa Romelu Lukaku aliyefunga matatu.

Mabao mengine ya Ubelgiji yamewekwa kimiani na Eden Hazard na Michy Batshuayi katika dakika ya 90.
Mabao ya Tunisia yamewekwa kimiani na Dylan Bronn katika dakika ya 18 ya kipindi cha kwanza na Khaziri dakika ya 90+3.

Msimamo wa kundi hilo unaonesha Ubelgiji ipo kileleni ikiwa na alama sita ikifuatiwa na England yenye pointi tatu ambapo Panama na Tunisia hazijapata alama yoyote.
Ubelgiji (3-4-3): Courtois 6, Alderweireld 6, Boyata 5.5, Vertonghen 6; Meunier 7.5, De Bruyne 7, Witsel 6, Carrasco 6; Mertens 6.5 (Tielemans 86) Lukaku 8 (Fellaini 59), Eden Hazard 9 (Batshuayi 67)
Goals: Hazard (6, pen 51), Lukaku (16, 45+3) , Batshuayi 90
Manager: R Martinez 7
Tunisia (4-3-3): Ben Mustapha 6; Bronn 6.5, Syam Ben Youssef 6, Meriah 5, Maaloul 5; Khaoui 6, Skhiri 6, Sassi 5.5 (Sliti 60 6.5); Fakhreddine Ben Youssef 6, Khazri 6, Badri 5
Goals: Bronn 18, Khazri 90+3
