
HIVI karibuni kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ilichafuka video mbalimbali ambazo zilikuwa zinamuonesha mwanamuziki ambaye yupo chini ya Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Mbwana Kilungi ‘Mbosso’ akicheza na wanadada jukwaani kana kwamba anafanya nao mapenzi.
Mashabiki mbalimbali walitoa maoni yao na wengi walimponda, mkali huyo wa Wimbo wa Futa huku wakidai kwamba bosi wake Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, ndiye anamharibu kwani mara nyingi hufanya vitendo hivyo.
Mikito Nusunusu, iliamua kumtafuta Mbosso ili kuzungumzia video hizo ambapo aliwaka na kudai kwamba kwake ni video za kawaida tu na wala hazina tatizo lolote na namna watu wanaozishadadia ni wabaya wake.
“Mimi sioni tatizo kiukweli, naona picha ni nzuri na hazina shida yoyote. Wabongo wakiona kitu wanachohisi ni kibaya hushika bango na kusahau vitu vya msingi,” alisema Mbosso.
Alipouliza juu ya kuitwa kwenye Baraza la Sanaa Tanzania (Basata), kutokana na video hizo, alisema hapendi kuzungumzia suala hilo zaidi kwani kwake halina mashiko yoyote!
Stori: Boniphace Ngumije.