Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka 2018/2019 imepita Bungeni baada ya kupigiwa kura na wabunge waliokuwepo Bungeni leo jioni, Juni 26, 2018.
Matokeo ya kura hiyo ni kama ifuatavyo; wabunge waliopiga kura 348, wabunge 43 hawakuwepo bungeni, kura za HAPANA 82, kura za NDIYO 266, hakuna kura iliyoharibika.