
Mbunge wa Tandahimba, Katani Hamad Katan, amesimama Bungeni kuchangia mjadala wa fedha za Export Levy za zao la Korosho ambazo wakulima wa zao hilo wanaotokea mikoa ya Kusini wanaidai ofisi ya Waziri wa Fedha na Mipango inayosimamiwa na Waziri Dkt Philip Mpanggo.