WATU watatu amefariki dunia na mmoja kujeruhiwa kufuatia ajali ya lori la mafuta mali ya Kampuni ya Transfuel Logistics Ltd Iringa (lenye namba za usajili T828 DCB) lililokuwa likitokea maeneo ya Ubungo kuelekea Mwenge kupoteza mwelekeo kisha kugonga kituo cha daladala cha Mlimani City – Dar es Salaam, leo Jumamosi, Novemba 23, 2019.

Kamanda wa Polisi Kinondoni, Mussa Taibu, amethibitisha watu watatu kufariki dunia na miili yao imehifadhiwa hospitali ya Mwananyamala Dar es Salaam.

Global TV Online, Global Publishers na +255 Global Radio imefika eneo la tukio na kushuhudia mazingira ya ajali hiyo ambapo majeruhi walikimbizwa pia katika hospitali ya.

Mashuhuda wameeleza kuwa baada ya gari hilo kumshinda dereva, liliparamia wafanyabiashara waliokuwepo eneo la karibu na kituo hicho cha mabasi na kusababisha vifo hivyo na dereva kutokomea kusikojulikana.

Kikosi cha uokoaji kimewahi kufika eneo la tukio na kudhibiti hali ya ajali hususani mafuta ambayo yangeweza kusababisha madhara makubwa iwapo yangelipuka. Hadi tunakwenda mitamboni, jeshi la polisi lilikuwa halijatoa kauli yoyote kutokana na ajali hiyo.
Endelea kufuatilia mitandao yetu ya Global Publishers, Global TVonline na + 255 Global Radio.