
WATU 20 wamefariki dunia na wengine 45 kujeruhiwa leo, Jumapili, Julai 1, 2018 eneo la Mbalizi, Mbeya, ambapo lori lenye kontena lilipoangukia daladala aina ya Toyota Hiace na kuyagonga mengine mawili kabla halijapinduka.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Mussa Taibu, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo eneo hilo ambako juhudi za uokoaji zilikuwa zinaendelea kwa kuihusisha kamati nzima ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Mbeya pamoja na wanajeshi wa Kambi la Mbalizi, ambayo ipo jirani na eneo la tukio.
