×

MAJI MAREFU AAGWA KARIMJEE DAR (PICHA + VIDEO)

Mwili wa  Steven Ngonyani ‘Maji Marefu’ ukifikishwa Karimjee.

WAZIRI Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa  leo amewaongoza viongozi mbalimbali wa serikali, wabunge na waombolezaji wengine kuuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Korogwe Vijijini, Steven Hilary Ngonyani (Khalid) maarufu Maji Marefu katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam.

 

Maji Marefu  alifariki usiku wa kuamkia jana (Jumanne) katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar alipokuwa akisumbuliwa na maradhi ya numonia.

Spika wa Bunge, Job Ndugai (kulia) akisalimiana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa,  baada ya kuzungumza machache jinsi alivyomfahamu marehemu.
Mmoja wa waombolezaji akilia kwa uchungu.
Wajane wa marehemu, Salma (kushoto) ambaye ni mke mkubwa na mke mdogo, Alwiya, wakiwa katika simanzi.

PICHA: RICHARD BUKOS | GPL