×

Mkutano wa Trump, Putin Watafuna Mamilioni!

 

MKUTANO kati ya  Rais Trump wa Marekani na Rais wa Urusi, Vladimir Putin, nchini Helsinki ‘umekula’ Dola 300,000 ambazo ni sawa na Sh. mil. 684 za Tanzania.

Fedha hiyo ni pamoja na manunuzi na matumizi mbalimbali kwa ajili ya mkutano huo nchini Helsinki.

Mkutano kati ya Trump na kiongozi wa Korea ya Kaskazini, Kim Jong-un, uliofanyika kama miezi miwili iliyopita, ‘ulikula’ Dola 162,000 ambazo ni sawa na Sh. mil. 369.