MWANASOKA Cristiano Ronaldo amewasili jijini Turin, Italia, kwa ajili ya mazoezi na timu yake mpya ya Juventus.
Mchezaji huyo raia wa Ureno na aliyenunuliwa kwa Paundi milioni 100 (Sh. bil. 300) na aliyekuwa mapumzikoni baada ya fainali za Kombe la Dunia, alipokelewa uwanjani na baadhi ya wachezaji wa timu hiyo.