×

Jerry Muro: Utalii Waimarika Arusha

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro.

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mh. Jerry Muro jana amemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. Mrisho Gambo katika kufunga mkutano wa wadau wa sekta ya Utalii.

Akifunga mkutano huo Mh.Muro amesema tayari serikali ya Mkoa imeanza kutatua changamoto zilizokuwa zinakabili wadau wa sekta ya Utalii ikiwemo adha ya kusimamishwa mara kwa Mara na askari wa usalama barabarani.

Pamoja na hayo pia serikali ya Mkoa imeanza kushughulikia Masuala ya kisera ambayo yalikuwa ni changamoto katika uendeshaji washughuli za Utalii

Katika masuala ya usalama Mh Muro kasema tayari Mkoa umeanza kutekeleza maoni ya wadau wa sekta ya Utalii yananyohusiana na watalii kwa kufungua Kituo cha Polisi chenye hadhi ya kimataifa ( Diplomatic ) kwa ajili ya kushughulikia masuala yote ya kiusalama yanahusiana na watalii

Akihitimisha hotuba yake Mh Muro amewakaribisha wadau wa sekta ya Utalii kuwekeza katika maeneo yanazunguka Mlima meru
Uliopo Wilaya ya Arumeru ambao ndio Mlima wa pili Tanzania kwa Urefu.

Mh Muro amemaliza kwa kusema Mkoa wa Arusha uko tayari kupokea na kuandaa mkutano Mkubwa wa kitaliii mwezi September mwaka huu.
#WakatiWetu #TanzaniaYetu #ArumeruYetu