









NAIBU Waziri wa Vijana, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza, usiku wa kuamkia leo, alijumuika na wadau wa filamu nchini katika Ukumbi wa Cinemax uliopo eneo la Mlimani City Jijini Dar, kuzindua filamu ya msanii, Duma iitwayo, Nipe Changu.
Shonza alisema wizara yake iko bega kwa bega na wasanii wa filamu ikiwemo kulinda haki zao na kuongeza kuwa haitamuacha pekee msanii yeyote anayehitaji msaaada wa kiserikali kwa kuwa fani hiyo imewapatia ajira vijana wengi hapa nchini.
Pia aliwataka wasanii hao kufanya kazi zao kiumakini ili kuwa na ubora wa kimataifa na kujizolea soko ndani na nje ya nchi ili wapate kunufaika na kipato.
(HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS / GPL)