MSANII wa filamu na Bongo Fleva, Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’, ametoa kituko cha mwaka baada ya kusema hakuna starehe anayoipenda kama kufanya tendo la ndoa na kwa wiki anaweza kufanya hata zaidi ya mara nne.
Akifafanua kauli yake mbele ya kinasa sauti cha Amani hivi karibuni, Baby Madaha alisema tendo hilo huwa anapenda kulifanya mara nyingi zaidi pindi anapokuwa na fedha mfukoni.
“Napenda kufanya nikiwa niko vizuri sana mfukoni, akili yangu yote iwe hapo tu yaani kwa wiki naweza kufanya hata zaidi ya mara nne,” alisema Baby Madaha.
Stori: Memorise Richard, Amani.