
MUIGIZAJI wa kitambo kwenye tasnia ya filamu Bongo, Skyner Ally ‘Skaina’ amewafungukia mastaa mbalimbali wanaokopa kwenye duka lake la nguo lililopo Kinondoni Studio jijini Dar na kusema kuwa kama hawatamletea fedha zake atawaweka hadharani maana kuna wengine hawampokelei hata simu na wengine wamemfungia kabisa asiwapate.

Akizungumza na Amani Skaina alisema anaumia kwa sababu anatafuta kwa taabu sana lakini anashangazwa na baadhi ya watu ambao wengine ni mastaa wanamkopa lakini mwisho wa siku wanamzungusha.
“Inaumiza, mtu unahangaika na jua huku na kule halafu mwingine anakuja kukukopa halafu anaingia mitini aisee inauma sana, nikiona inazidi kwa kweli nitawachana live kabisa maana wengine wana majina makubwa lakini wanajitia kichwa ngumu,” alisema Skaina.
Stori: Memorise Richard, Amani.