×

Tambwe: Makambo Ni Zaidi Ya Ngoma

Mshambuliaji wao mpya raia wa DR Congo, Heritier Makambo.

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe amewataka wapenzi na mashabiki wa timu hiyo kutokuwa na wasiwasi na uwezo wa mshambuliaji wao mpya raia wa DR Congo, Heritier Makambo na amewahakikishia kuwa yupo vizuri zaidi ya alivyokokuwa Mzimbabwe, Donald Ngoma ambaye sasa yupo na kikosi cha Azam FC.

 

Tambwe ambaye ana rekodi nzuri ya kuzifumania nyavu klabuni hapo tangu alipojiunga timu hiyo msimu wa 2014/15 akitokea Simba, amefikia hatua hiyo baada ya baadhi ya mashabiki wa timu hiyo kuufananisha uwezo wa Makambo na ule aliokuwa nao Ngoma wakati akiitumikia timu hiyo.

“Mwili wake (Makambo) umeonekana ‘kunoki’ kutokana na mazoezi magumu ambayo alikuwa akifanya tulipokuwa Morogoro. Anahitaji mechi nyingine mbili za ushindani ili aweze kuwa sawa, kwa jinsi ninavyomuona atafanya mambo makubwa zaidi ya alivyokuwa Ngoma.

 

“Anajua kupiga mashuti, anajua kufunga kwa kichwa na miguu, ana uwezo wa ku­kaa na mpira, anajua kutengeneza nafasi za kufunga lakini pia siyo mchoyo na kutoa pasi za kufunga kwa wenzake, lakini pia ana kasi kubwa na nguvu za kupambana na mabeki, kwa hiyo mashabiki wampatie muda tu, naamini wote tutafurahia kuto­kana na uwezo wake,” alisema Tambwe.