×

BREAKING NEWS: MAMA MZAZI WA SUGU AFARIKI DUNIA

Taarifa zilizotufikia hivi punde, zinaeleza kwamba mama mzazi wa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu), amefariki dunia asubuhi ya leo, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, kwenye wodi ya wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU) alikokuwa akitibiwa.

 

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Msemaji wa Hospitali ya Muhimbili, Aminiel Eligaesha, marehemu alikuwa amelazwa wodi namba 18 na hali yake ilibadilika usiku, na kulazimisha ahamishiwe ICU alikofariki asubuhi ya leo.

Sugu akiwa na mama yake enzi za uhai wake.

Taarifa zaidi zitaendelea kukujia kupitia hapahapa.