
MBUNGE wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu), ameshindwa kujizuia na kujikuta akiangua kilio na kumwaga machozi alipokuwa akisoma wasifu wa marehemu mama yake, Bi. Desderia Lungu Mbilinyi leo Jumanne, Agosti 28, 2018 wakati wa ibada ya kuaga mwili wa mama huyo katika Kanisa Katoliki lililopo ndani ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Bi. Desderia Mbilinyi alifariki dunia juzi Jumapili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa kwenye wodi ya wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU) akipatiwa matibabu.
Baada ya kuaga mwili wa marehemu umesafirishwa leo kwenda nyumbani kwake, jijini Mbeya kwa ajili ya maziko.
Edwin Lindege | Global Publishers