×

Kampuni ya Mafuta Yazuiwa Kuchukua Pesa Kwenye Benki

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam imezuia kwa muda Kampuni ya Alchemist Energy Trading DMCC ya Dubai kuchukua pesa kwenye barua ya mkopo (letter of credit) baada ya kushinda tenda namba PBPA/CPP/PMS/C3-KOJ1/02/2021 iliyotangazwa na Wakala Serikali wa Uagizaji wa Mafuta ya Pamoja (PBPA).

 

Katika kesi hiyo ndogo ya zuio, imeelezwa kuwa mshitakiwa ambaye ni Alchemist Energy Trading DMCC alishinda tenda hiyo na baada ya hapo alitakiwa kuleta mafuta nchini kulingana na masharti ya tenda hiyo, lakini alishindwa kufanya hivyo.

 

Katika uamuazi huo uliosomwa mbele ya Jaji Leila Edith Mgonya, kampuni hiyo tayari ilikuwa imeshaanza kuchukua pesa kutoka kwenye baadhi ya mabenki bila kuingiza mafuta nchini kinyume cha masharti ya tenda hiyo. Shauri la msingi la keshi hiyo linaendelea mbele ya chemba ya Kimataifa ya Kibiashara (ICC).

 

Leave a Comment