
MSANII wa Bongo Movies na muziki wa Injili, Rose Alphonce ‘Muna’ amesema kwamba kitendo cha yeye kuonekana akiwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu na wenye magonjwa mbalimbali ni kazi anayoifanya kumuenzi marehemu mtoto wake Patrick kwa sababu alikuwa na upendo na watoto wenzie.
Akizungumza na Amani mapema wiki hii, Muna alisema kwa sasa watu wengi wamekuwa wakimuona akifanya shughuli mbalimbali za kusaidia wenye uhitaji, kazi ambayo ataifanya kwa kadiri ya uwezo wake wote kumuenzi marehemu mwanaye.
“Nafanya hivi kwa sababu ni maono toka kwa Mungu, pia naona ndio njia pekee ya kumuenzi mtoto wangu kwa sababu yeye alikuwa na upendo na watoto wenziye, ilikuwa ukimpa kitu ale, hawezi kula lazima ampe na mwenziye na hata kama kipo kimoja basi yeye hatakula atampa mwenziye,” alisema Muna ambaye mwanaye alifariki miezi kadhaa iliyopita nchini Kenya