MWANAMUZIKI wa kike ambaye pia ni mama wa mtoto mmoja, Aika Mariale wa Kundi la Navy Kenzo ametamba kuwa na uwezo wa kufanya vitu vingi kwa wakati mmoja na si kutegemea muziki tu.
Katika mahojiano na Ijumaa Wikienda, Aika alisema kwa sasa anafanya kazi tofauti za kijamii kama kuwakusanya watoto wa mitaani ambao wanaweza kucheza michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu.
“Pamoja na kuwa mimi ni mwanamuziki na mama pia namuomba Mwenyezi Mungu anisaidie jukumu hili lingine la kuchukua watoto wa mitaani na kuunda timu ili waweze kushindana na kuonesha vipaji ili baadaye wacheze kwenye timu kubwa,” alisema Aika.
Stori: Neema Adrian, Dar