×

Simbachawene Amvaa MSIGWA “Unatafuta Chuki Tu” – Video

Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema) Mchungaji Peter Msigwa amesema uamuzi wa Serikali kuhamia Dodoma haukuwa sahihi kwasababu si kipaumbele cha Taifa. Amesema pia jambo hilo halimo katika mpango wa Taifa wa Maendeleo wa miaka mitano.

 

Akizungumza bungeni leo Jumanne Septemba 4, 2018 katika mjadala wa muswada wa sheria ya kulitangaza Jiji la Dodoma kwa Makao Makuu ya nchi mwaka 2018, Mchungaji Msigwa amesema kuifanya Dodoma kuwa makao makuu ni dhana nzuri lakini kuna tofauti kubwa ya kufanya jambo zuri na sahihi.

 

Akijibu hoja hiyo, Mbunge George Simbachawene amesema anachikifanya Msigwa nisawa na kiutafuta chuki kwani tayari ofisi zote kuanzia Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Mawaziri na viongozi wengine wameshahamia Dodoma amebaki Rais Magufuli pekee hivyo zoezi hilo limekamilika kwa asilimia 99.

Aidha, amesema jambo la kuhamia Dodoma lilianza tangu ukononi na awamu nyingine zauongozi lakini Rais Magufuli ametelekeza kwa vitendo hivyo anapaswa kuungwa mkono.