
USIKU wa kuamkia leo ilikuwa ni shangwe kwenye Ukumbi wa Mlimani City wakati wa sherehe ya Rapper nguli wa Bongo ambaye pia ni Mbunge wa Mikumi Joseph Haule ‘Profesa Jay’ aliyefunga ndoa jana hiyohiyo Julai 8, 2017 na mpenzi wake Grace katika Kanisa la St. Joseph lililopo Posta ya Zamani Dar.

Katika sherehe hiyo ilihudhuriwa na watu maarufu kibao wakiwemo wabunge, wasanii wa muziki, filamu na komedi pamoja na viongoizi mbalimbali wa serikali na vyama vya siasa.

Katika kusherehekea harusi hiyo, wakati wa kuingia ukumbini Prof. Jay aliingia akiimba wimbo wake wa ‘Kamili Gado’ huku akiwa amemshikilia mkewe, Bi. Grace, wimbo ambao uliamsha hisia kwa waalikwa wakiwemo wabunge Mch. Peter Msigwa na Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ambao walionekana kucheza kwa nguvu zote kumsapoti mbunge mwenzao.

Global Publishers ilifanikiwa kunasa picha kadhaa wakati sherehe hiyo ikianza na waalikwa wakiingia ukumbini pamoja na maharusi wenyewe.


PICHA NA RICHARD BUKOS | GLOBAL PUBLISHERS
==============