
Rais Dkt John Magufuli, ameendelea na ziara yake ya kutembelea, kukagua na kuzindua miradi mbalimbali inayotekelezwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini na leo ametembelea shule ya msingi Mwisenge mjini Musoma aliyosoma Baba wa Taifa , Mwl Julius Nyerere.
Baada ya hapo, Rais Magufuli akafanya mkutano wa hadhara na kuzungumza na Wananchi katika viwanja vya Mkendo.
“Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere angekuwa amezaliwa Ulaya, tungekuwa tunakwenda kutalii kule, lakini sisi Watanzania hatuthamini vya kwetu, nimeagiza shule aliyosoma Mzee Nyerere iboreshwe, iwekewe uzio.
“Nimebadilisha mawaziri wa maji mara nyingi lakini wananchi wa Bunda bado wanabunda na hawana maji, aliyehujumu mradi huo yupo hapa Musoma, lakini ameshika vyombo vya dola, amelipwa bilioni zote tisa, ninafahamu.
“Ndiyo maana niliomba urais ili niwale wao waliokuwa wanakula pesa za miradi, kama waliona utamu wa kula pesa zetu nao waone uchungu wa kuliwa. Mimi wananisema ni mkorofi, jamani mimi ni mpole mnoo, hata ungekuwa wewe unamkuta mama mwenye miaka 100 analia ametapeliwa aridhi, utaacha kumhurumia.
“Waliohujumu mradi huu wa maji Musoma walilipwa pesa karibu zote, Wizara ya maji ipo, viongozi wapo, kwa nini msimgesondeke ndani wasote huko hata miaka 3? Niwaombe viongozi niliyowateua mbadilike, ninataka watu wa Musoma.
“Nimepata taarifa Mkuu wa wilaya ya hapa (Musoma) amewakataza wananchi wasibebe mabango akiwatisha atawasondeka ndani. Mtu nimemteua mini, yupo kwenye ofisi zenye bendera ya CCM, lakini hataki wananchi wanieleze kero zao,” alisema Magufuli.