×

Waziri Aweso ashiriki Mkutano Maalum wa Huduma ya Maji Duniani

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ameshiriki Mkutano Maalum unaohusiana na masuala ya Huduma ya Maji Duniani wa World Water-Tech Innovation Summit (WWIS) 2023 nchini Uingereza.

 

Katika mkutano huo unaoratibiwa na serikali ya Uingereza, Waziri Aweso ameambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga na Ujumbe wa Wizara ya Maji kutoka Tanzania.

 

Wakiwa kwenye Mkutano huo, Waziri Aweso na Katibu Mkuu wa Injinia Sanga wametoa wito kwa wadau wa Sekta ya Maji duniani kuzidisha jitihada katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwani hii ni changamoto inayokabili dunia nzima.

 

Waziri Aweso amesisitiza; “Tanzania tunaendelea kuhimiza juu ya utunzaji wa vyanzo vya maji pamoja na kuwekeza katika uvunaji wa maji ya mvua kwa ujenzi wa mabwawa ili kuhakikisha yanakuwa sehemu ya kukabiliana na changamoto hii ambao pia wametoa fursa mbalimbali zilizopo katika Wizara ya Maji ikiwa ni pamoja na maeneo yanayotakiwa kufanyiwa kazi kwa mashirikiano na wadau.”

 

Katika hatua nyingine, Mkutano huu umekuwa na mjadala wenye kutoa suluhu ya pamoja ya namna bora ya kuboresha mifumo ya usambazaji majisafi na usafi wa mazingira nchini (Majitaka) kwa kuendana na ongezeko la watu hasa maeneo ya mijini na kujadili suluhu ya kukabiliana na changamoto ya upotevu wa maji inayoikabili nchi mbalimbali duniani na mwisho mjadala juu athari ya mabadiliko ya Tabianchi.

Leave a Comment