×

Mkongo Yanga Aikejeli Simba

Mwinyi Zahera

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera ameeleza dhamira yake ya kuhakiki­sha anafanya vizuri msimu huu kwa ku­hakikisha anashinda kila mechi atakayo­cheza, huku akisema haifuatilii Simba.

 

Zahera kwa sasa yupo na timu ya taifa ya DRC Congo ambapo ni kocha msaidizi iliyopo nchini Liberia kuvaana na timu ya taifa ya nchini humo katika mechi za Kuwania kushiriki Afcon keshokutwa Jumapili usiku.

 

Yanga kwa sasa ipo nafasi ya 10 ya msimamo wa ligi kwa kuwa na pointi tatu ikiwa na michezo miwili mkononi, baada ya kucheza mechi moja tu.

Kikosi cha timu ya Yanga.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Zahera kutoka Liberia, amesema kuwa, anachohitaji ni kuona timu yake inafanya vizuri kwenye ligi na ikiwezekana kushinda kila mchezo ili kuweza kujiweka katika nafasi nzuri ya msimamo wa ligi.

 

“Ligi ni ngumu na ina ushindani wa hali ya juu, tunahitaji kufanya vizuri katika mechi tutakazocheza, nitakiandaa kikosi changu kuona tunafanikiwa kushinda kila mechi ili tuweze kuwa juu, kuhusu Simba siwezi kuizungumzia kwa kuwa siifuatilii hata kidogo, nazifuatilia timu nyingine.

 

“Nimeandaa programu ambazo zinaendelezwa kipindi hiki chini ya kocha msaidizi, naamini kila kitu kitakwenda sawa,” alisema Zahera ambaye familia yake inaishi Ufaransa.