AJALI mbaya imetokea katika mteremko mkali wa Iwaranje maeneno ya Igawilo leo Ijumaa, Septemba 7, 2018 ikihusisha malori matatu ya mafuta, Hiace ya abiria na gari moja ya mizigo.

Katika ajali hiyo watu 11 wamedaiwa kupoteza maisha huku kadhaa wakijeruhiwa na kukimbizwa hospitali kwa matibabu.

RPC wa Mbeya, Urich Matei amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo imeelezwa kuwa chanzo ni kufeli breki kwa gari mojawapo.

