
NAIBU Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru), Brigedia Jenerali John Mbungo ameweka wazi kuwa yeyote atakayewapata Mwenyekiti wa zamani wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe na mwenzake Frank Lauwo atapata zawadi nono.
Hans Poppe na Lauwo wanatafutwa ili waunganishwe kwenye kesi ya kutoa taarifa za uongo akishirikiana na viongozi wengine wa Klabu ya Simba, Rais Evans Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’.

Viongozi hao wanakabiliwa na kesi ambayo inasikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar, ambapo jana ilishindwa kuendelea kwa watuhumiwa hao wawili kutokana na mwendesha mashitaka wa Takukuru kutokuwepo mahakamani hapo.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, jana, kwenye Makao Makuu ya Takukuru, Mbungo alisisitiza kuwa kwa mtu yeyote atakaye fanikisha kupatikana kwao atapewa zawadi nono.
Washitakiwa hao wanatafutwa na taasisi hiyo ili wafikishwe mahakamani kujibu kesi ya jinai ya namba 214/2017 ya Jamhuri dhidi ya Aveva, Kaburu iliyopo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
“Poppe anatafutwa kwa kosa la kutoa taarifa za uongo kuhusiana na malipo ya kodi, kifungu 106(1)A& C(i) cha Income Tax Act sura ya 332 R.F 2008, kwamba kati ya Machi 10, 2016 na Septemba 30, 2016.
“Mshitakiwa akishirikiana na wenzake Aveva na Kaburu walitoa maelekezo ya uongo kwenye Ofisi za Mamlaka ya Mapato