GLOBAL TV ONLINE imefanya mahojiano maalum na mama mzazi wa muigizaji maarufu Bongo ambaye kwa sasa ameokoka, Rose Alphonce ‘Muna Love’, anayeitwa Bi Moyo na amezungumzia ukweli wote kuhusiana na maisha ya binti yake huyo huku akisisitiza kwamba yeye ndiye mama mzazi wa Muna, tofauti na mwenyewe anavyoeleza kwamba siyo mama yake mzazi.

Pia dada wa Muna Love, Eva Nungu amefunguka kuhusiana na ukweli anaoufahamu juu ya madai ya mtoto mwingine wa Muna anayeishi kijijini Moshi aitwaye Brian na kueleza kuwa ni mtoto wa kwanza wa Muna japokuwa mwenyewe hataki jambo hilo lifahamike.
Eva amesema mtoto huyo alizaliwa mwaka 2005 katika Hospitali ya Palestina iliyoko Sinza na baba wa mtoto huyo anatambulika kwa jina la Fredy. Amesema Muna aache kuigiza kwani ameokoka hivyo anapaswa kuwa mkweli.