
Rais wa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Akishiriki Baraza la Eid El-Fitr Ukumbi wa JNICC Dar es salaam, tarehe 31 Machi, 2025.
Viongozi wa dini nchini wametakiwa kutumia nyumba za ibada (Misikiti na Makanisa) kuendelea kuwakumbusha na kuwaelimisha waumini umuhimu wa kumtumikia Mwenyezi Mungu kama wanavyofanya mara zote, sambamba na kuhubiri umuhimu wa kutunza amani katika nchi.

Rai hiyo imetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati akihutubia Baraza la Eid El-fitr kitaifa, hafla iliyofanyika jioni ya Jumatatu Machi 31.2025 ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam ambapo katika maelezo yake ameweka wazi kuwa serikali haitovumilia viongozi wa dini wanaotumia nyumba za ibada kusambaza chuki dhidi ya serikali sambamba na kuhubiri uvunjifu wa amani kwenye nchi.
Sambamba na hilo, Rais Samia pia ametoa wito kwa viongozi wa dini kutoruhusu kutumika kisiasa badala yake wajikite kwenye majukumu yao ya kila siku.


