×

Bikosports yampa bonasi ya sh. Mil 5 mkazi wa Kigamboni

Balozi wa Bikosports, Maulid Kitenge akizungumza jambo katika hafla hiyo ya kumkabidhi mshindi.
Balozi wa Bikosports, Maulid Kitenge (wa tatu kushoto)  akikabidhi hundi ya sh Milioni 5 mshiriki wa bahati nasibu ya kubashiri matokeo ya michezo ya mpira wa miguu, Salum Juma wa pili kutoka kulia.

 

 

MKAZI wa Kigamboni, jijini Dar es Salaam, Salum Juma, ameibuka kidedea baada ya kukabidhiwa Sh Milioni 5 kutoka kampuni ya michezo ya kubashiri matokeo ya bikosports, baada ya mdau huyo wa michezo ya kubahatisha kutabiri michezo 11 ya mpira wa miguu duniani, jambo lililowavutia Bikosports na kuamua kumpa bonasi kama sehemu ya kuwajali wachezaji  wa bahati nasibu yao.

 

 

Akizungumza katika Mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Biko sports, Jeff Lea alisema kitendo cha shabiki huyo kubashiri michezo 11 kimewafanya waone haja ya kumpa bonasi, akiamini kuwa haitawavunja nguvu wasahiriki wao badala yake itawapa mwamko katika kushiriki mbio za kuwania Sh Milioni 97 kwa mtu atakayeibuka shujaa wa kubashiri michezo 13 kama droo yao kubwa inavyotaka.

 

 

Leya alisema licha ya wadau mbalimbali kuendelea kuvuna fedha mbalimbali kwa kubashiri na Kampuni yao ambayo namba ya kampuni ni 101010, ambapo mchezo huo unaweza kuchezwa kwa kutuma jamvi kwa *149*89# bila kusahau kwa kuingia kwenye mtandao wao moja kwa moja kujionea mpangilio mzima wa mchezo wao unaoweza kuchezwa bila kuwa na akaunti huku ushindi ukipatikana moja kwa moja kwenye simu ya mkononi.

 

 

“Biko Sports tunawajali sana wateja wetu ndio maana leo tumeamua kwa dhati kabisa kumpa bonasi ya Sh Milioni tano ndugu yetu Juma kwa sababu amejitahidi kwa kubashiri michezo 11, akishindwa miwili tu ili avune Sh Milioni 97 kutoka kwetu, ambapo bikosports ina machaguo Zaidi ya 125.

 

“Biko Sports ni rahisi kubashiri na kushinda bila kusahau jinsi tunavyojali wateja, hivyo kwa pamoja tunaamini watanzania wataendelea kubashiri kwakupitia kampuni yetu kwa sababu tumeboresha mno huduma zetu na fedha zetu zinalipwa muda mfupi tu baada ya kufanikiwa kushinda kwenye jamvi husika,” alisema.

 

 

Naye Balozi wa Biko Sports Tanzania ambaye ni mwandishi nguli wa michezo nchini hapa nchini, Maulid Kitenge, alimpongeza Juma kwa kuonyesha shauku ya kuzitafuta Sh Milioni 97 za Bikosports, huku akiwataka Watanzania wote na wapenda michezo ya kubashiri matokeo kucheza kwa kupitia kampuni yao yenye uhuru wa mechi nyingi na za kutosha.

 

 

“Ukiwa ni mdau wa michezo hii ya kubashiri matokeo, hapana shaka Bikosports ndio mahala sahihi na tulivu mno kwa kushinda zawadi mbalimbali pale mtu anapofanikiwa kushinda jamvi lake, hivyo hata kwa hatua hii ya kutoa bonasi kwa watu wanaofanya vizuri kutabiri kwetu ni shauku ile ile ya kuwajali wateja wetu.

 

 

“Watanzania wachangamkie kubashiri kwenye kampuni ya Biko Sports kwa sababu kuna mpangilio mzuri na yoyote anaweza kubashiri matokeo hata kwa kutumia simu ya tochi au kwa kupitia mtandao wetu wa www.bikosports.co.tz, “alisema.

 

 

Akizungumzia hatua ya kupewa bonasi yake ya Sh. Milioni tano, mshindi huyo aliishukuru bikosports kwa kumpa bonasi hiyo akisema kuwa itaendelea kumfanya aendelee kuziwinda fedha nyingi kutoka bikosports hususan sh milioni 97 ambazo zitatoka mtu akifanikiwa kubashiri michezo 13.

 

 

“Lengo langu ni kupata hizo zawadi za juu kabisa, hivyo kupewa bonasi hii ni jambo zuri kwangu, ila nitahakikisha nashinda dau hilo kubwa, nikiamini kuwa linawekea mwangaza mzuri wa kimaisha kwa kupitia bahati nasibu hii ya kubashiri matokeo kutoka kwenye kampuni ya bikosports,” Alisema Juma na kuwataka Watanzania waendelee kubashiri kwa kupitia bikosports ili wavune zawadi mbalimbali.

 

 

Bikosports ni mchezo mzuri na rahisi unaotoa nafasi nyingi Zaidi ya ushindi, ukichezeshwa nchini Tanzania, ambapo wateja wanaweza kubashiri kuanzia mchezo mmoja na kuendelea, ambapo kwa wale watakaofanikiwa kubashiri michezo 13 kwa pamoja, watajishindia jumla ya Sh Milioni 97, huku kianzio cha fedha cha kubashiri kikianzia Sh 500 na kuendelea.