×

MV NYERERE: Kilio cha Watoto Walipoona Kaburi la Mama Yao – VIDEO

MOJA kati ya miili mitano ya watu walipoteza maisha katika ajali ya MV Nyerere na kuzikwa juzi Jumapili, Septemba 23, katika makaburi ya pamoja eneo la Bwisya, Ukara Ukerewe umetambuliwa na mume wake Matindi Mabere na hivyo serikali kulikabidhi rasmi kaburi kwa familia yake.

 

Kaburi ambalo ulizikwa mwili huo umetambuliwa kuwa ni wa mama Buleba Matindi mkazi wa Kijiji Kimwani wilayani Muleba Mkoani Kagera.

 

Kaburi hilo limekabidhiwa kwa familia na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jennister Mhagama kwa kushirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Kigoma Malima.

LIVE: Kilio cha watoto walipoona kaburi la mama yao!