×

Mtendaji Azilongwa Amuunga Mkono Rais Samia na Royal Tour

Mtendaji wa Kata ya Huzi wilayani Chamwino Azilonga Bohari ametembelea Hifadhi ya Wanyama ya Ngorongoro akiwa pamoja na vijana wengine wa UVCCM.

MTENDAJI wa Kata ya Huzi Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma Azilongwa Bohari akiwa na Vijana wenzake wa UVCCM wametembelea Ngorongoro National Park kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan Kwa Royal Tour.

 

Wakiwa huko walifurahi na kufarijika sana kwa wingi wa watalii wa ndani na nje.

Mtendaji Azilonga amesema anaunga mkono juhudi za Rais Samia za ukuza Utalii nchini

Rais Samia kupitia Filamu yake ya Royal Tour amehamasisha kwa asilimia kubwa watalii wa ndani na nje ya nchi kutembelea maeneo mbalimbali ya vivutio vya utalii nchini ambayo kimsingi inasaidia kuongeza mapato kwa wananchi wa maeneo husika lakini pia pato la Taifa kwa ujumla.

Leave a Comment